Ikiwa ni visa vinavyotokea nadra na kushtua, mama mmoja mwenye umri wa miaka 31, kutoka Mkoa wa Ntungamo nchini Uganda, aliachwa akitahayari baada ya mume wake kumkimbia alipopata taarifa kuwa wamepata pacha wanne hospitalini.

Mume huyo, Asiimwe Elkangiro, anaripotiwa kutoroka na kuzima simu baada ua kufahamishwa kuwa mkewe alitakiwa kufanyiwa upasuaji ili ajifungue pacha hao wanne ambao wote ni wa kike.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily monitor la Uganda, Elkangiro, ana wake mwenye wake wengi, ikiwa mke huyu aliyejifungua sasa alikua ni mke wa tatu, ambaye tayari alikuwa amezaa mtoto mmoja.

Mhudumu wa afya katika Hospitali ya Kisiizi alisema Mary Kyomugisha ambaye ndie mama wa pacha hao alisumbuliwa kiakili alipogundua kuwa kuwa mume wake amemkimbia.

Kutokana na tukio hilo Mary aliwaomba wasamaria wema kumsaidia kulipa bili ya hospitali ambayo ni zaidi ya KSh 40,000, mahitaji ya watoto hao kama vile maziwa sababu hana uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha kwa kuwa titi lake moja lina matatizo hivyo haliwezi kutoa maziwa.

“Watoto wanalia kila mara kwa sababu siwezi kutoa maziwa ya kutosha. Titi langu moja lina tatizo kwa hivyo linategemea titi lingine. Mume wangu hana msaada na kumudu maziwa ni ngumu,” alisema Kyomugisha.

Mkuu wa hospitali hiyo Moses Mugume, alisema upasuaji huo ulifanywa katika wiki ya 32 na watoto hao wamewekwa kwenye kiatamazi huku mkubwa zaidi akiwa na uzani wa kilo 1.6.

Twitter yarejea baada ya miezi saba
Nabi asitisha mapumziko, awaita wachezaji kambini