Huko Kusini Mashariki mwa China mji wa Chongqing watoto 14 wa chekechea wamejeruhiwa vibaya na kisu wakiwa shuleni kwao.

Polisi wamesema kuwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 39 aliingia katika shule yao na kisu na kuanza kuwajeruhi watoto hao waliokuwa wakicheza katika uwanja wao  wa michezo.

Lengo la mwanamke huyo kufanya hivyo bado halijafahamika, japokuwa baadhi ya ripoti kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa mwanamke huyo ana dukuduku kubwa na serikali hivyo anafanya kisasi.

Mwanamke huyo mwenye jina la ukoo, Liu alitiwa mbaroni palepale alipofanya tukio hilo la kikatili kwa watoto wa chekechea.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha watoto hao waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa shuleni huku wengine wakiwa wamechanwa chanwa vibaya usoni.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni ikidai kuwa kufuatia tukio hilo watoto wawili wamefariki dunia kitu ambacho polisi wamepinga taarifa hizo za vifo na kusema watu wapuuze taarifa hizo na kuwataka wasizisambaze kwani hazina ukweli.

Matukio ya kikatili yamekuwa hadimu sana China, aidha kumekuwa na matukio ya watoto kutekwa kwa visa vinavyodaiwa kuwa ni kisasi.

Aprili mwaka huu watoto 9 waliuawa vibaya mara baada ya kuvamiwa na kijana mwenye umri wa miaka 28 walipokuwa njiani kuelekea nyumbani, kwa kisa alichodai kuwa pindi alipokuwa anasoma alikuwa akizomewa na wanafunzi wenzake hivyo ameamua kurudisha kisasi.

Mtuhumiwa huyo wa mauaji ya watoto 9 amehukumiwa mapema Septemba mwaka huu.

 

UVCCM kuajiri vijana 300, wadai BAVICHA sio saizi yao
Google yawafukuza kazi wakurugenzi kwa kashifa ya ngono