Watoto wa Uganda waliong’arisha video ya ‘Unforgettable’ ya French Montana wanaojulikana kama Ghetto Kids, wametangaza neema waliyojaliwa mwaka huu ya kununuliwa jumba la kifahari na mwanamuziki huyo.

Montana ambaye jina lake halisi ni Karim Kharbouch amefanikisha ndoto hiyo ya Triplets Ghetto Kids ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kuwapandisha kwenye jukwaa la Tuzo za BET nchini Marekani. Video ya ‘Unforgettable’ imeangaliwa zaidi ya mara Milioni 798.

Watoto hao wameandika, “mwaka 2018 ulikuwa mwaka mzuri. Tunamshukuru Mungu kwa baraka, tunamuomba aendelee kutubariki zaidi na zaidi,”

“French Montana na timu yote, hatuna maneno yanayotosha kuwashukuru! Tunawaombea tu Mungu aendelee kuwabariki na tutaendelea kujivunia kuwa nanyi,” wameongeza.

Jumba la Ghetto Kids

Kundi hilo ambalo lilianza kuonekana kwenye ulimwengu wa burudani kupitia video za Eddy Kenzo, pia wamewashukuru Mungu pamoja na mashabiki wao.

Montana amewahi kuwabariki wananchi wa wilaya ya Iganga nchini Kenya kwa kuwajengea hospitali ya Suubi ambayo inatibu zaidi ya watu 20,000.

Ali Kiba kudhamini Wasafi Festival, Diamond aridhia
Prof. Mbarawa atoa onyo kali kwa watendaji wa mamlaka za maji

Comments

comments