Watoto wawili wa familia moja waliopotea kwa siku moja wamepatikana wakiwa wametenganishwa kichwa na mwili na miili yao imekutwa imetelekezwa kichakani katika kijiji cha Mashule wilayani Bukoba Mkoani Kagera

Majina ya watoto hao ni Auson Respikius(7) na Alistidia Respikius(5) walioondoka nyumbani Oktoba 21 majira ya saa 10 jioni kwenda kutembea na mtoto wa jirani.

Baba yao ameeleza kuwa ilipofika majira ya saa 12 jioni yeye na mkewe walianza kuwatafuta hadi kwa jirani ambapo walimkuta mtoto waliyeenda nae amerudi

Mtoto huyo alieeza kuwa alipotezana na watoto hao baada ya yeye kuingia dukani kununua biskuti.

Baba alisema alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji na Kitongoji

Waliwatafuta hadi usiku wa saa nane bila mafanikio, waliahirisha hadi kesho yake asubuhi ambapo waliwakuta watoto hao kichakani wakiwa wamefariki

Rwanda kinara watu kuishi miaka mingi EAC
Video: NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba

Comments

comments