Watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu na miaka sita, raia wa Afrika Kusini wamefungua mashtaka dhidi ya kanisa la The Synagogue Church of All Nation (SCOAN) la mhubiri maarufu nchini Nigeria, TB Joshua.

Watoto hao wamechukua uamuzi huo kufuatia kifo cha baba yao, aliyekuwa mmoja kati ya watu 106 waliopoteza maisha katika tukio la kuanguka kwa jengo la kanisa hilo lililokuwa katika hatua ya ujenzi, mwaka 2014.

Watoto hao wanatafuta kulipwa fidia ya $520,000 ( sawa na shilingi za Tanzania 1,137,318,000) wakieleza kuwa ni kiasi ambacho endapo baba yao angeweza kutumia kuwasaidia kimahitaji hadi ambapo angefika umri wa miaka 70.

Jengo

Mwanasheria wa watoto hao, Bolaji Ayorinde ameiambia BBC kuwa amekuwa akipokea maombi mengi ya ndugu wa watu waliofariki kwenye ajali hiyo ya kuangukiwa na na jengo la kanisa hilo wakitaka kuchukua hatua za kisheria.

Hata hivyo, hakuna aliyemfungulia mashtaka TB Joshua binafsi isipokuwa wahandisi waliokuwa wanasimamia jengo hilo ndio wanaokabiliwa na kesi mahakamani.

Kanisa hilo limekuwa likieleza kuwa ndege ndogo iliyokuwa ikizunguka juu ya jengo hilo ndio chanzo cha kuanguka kwake na sio vinginevyo.

Hongera Dk. Kikwete, ila unapozima moto wa Libya zikumbuke ‘Cheche’ za Zanzibar
Gerad Ajetovic Awasili Tanzania Kumabili Francis Cheka