Watu 10 wamenusurika kifo mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya boti waliyopanda kuzama kwenye bahari ya Hindi Jijini Tanga wakati wakiwa wanaenda kuangalia visiwa vilivyopo majini.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 ambapo watu hao walikuwa wamepanda boti waliyokodi kutoka eneo la Yanchi Club.

Amesema kuwa baada ya watu hao kupanda boti hiyo walikuwa wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo na ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka ndipo ilipopinduka.

“Watu hao walikuwa wametokea eneo la Yanchi Club walikuwa wanakwenda kutembelea visiwa mbalimbali vya bahari ya hindi wakati wakiwa njiani upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi wakapinduka,“amesema kamanda Bukombe

Aidha, Kamanda Bukombe amesema kuwa kwenye boti hiyo iliyokuwa na watu 11 ambapo 10 kati yao waliweza kuokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwingine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo mpaka sasa hajulikani alipo.

“Natoa wito kwa wananchi wanaotumia bahari kusafiria kuchukua tahadhari wanapokuwa baharini kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa “amesisitiza Kamanda Bukombe

LIVE: JAMES MBATIA AKIZUNGUMZIA AJALI YA LORI MOROGORO
Video: Magufuli Tusiwe wepesi wa kuhukumu, Vigogo Serikalini roho juu ajali ya Morogoro