Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma, Mwanahamisi Munkunda amesema watu zaidi ya 1000 wilayani humo hawana makazi kutokana na nyumba 237 kubomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini humo.

Munkunda  amewataka Wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kupita kwenye mito ambayo imefurika.

Pia amewataka wazazi kuhakikisha watoto hawachezi mitoni na kwenye madimbwi yaliyojaa maji

Ni baada ya kuzuru maeneo yaliyoathiriwa na mvua, Mkuu huyo wa wilaya amesema pamoja na kubomoka  kwa nyumba, mvua pia zimeharibu miundombinu ya barabara ambapo ametaja maeneo yaliyoathiriwa kuwa ni Bahi Sokoni, Bahi Misheni, Mji Mpya na Nkogwa, na Vijiji vya Mbuyuni, Uhelela, Laloi, Mugu na Nagulo.

Aidha, ameeleza kuwa wameomba Milioni 400 ili kukarabati miundombinu iliyoharibika ikiwemo madaraja, na tayari fedha hizo zimepatikana na zitaanza kutengeneza miundombinu hiyo ili kuhakikisha shughuli mbalimbali za kiuchumi hazisimami kwasababu ya mvua.

Padri aliyefungisha ndoa ya Stamina afunguka
Ndoa si siri tena, Lisa amuanika hadharani mume wake Mabeste, ''Ana mkono wa kupiga, si mtafutaji''

Comments

comments