Takribani watu 19 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi waliokuwa wakisafiria kugongana na gari la mizigo katika barabara ya Mbaruk, Naivasha, Kenya.
 
Kamishna wa usalama barabarani, Zero Salome amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu, basi la abiria pamoja, gari ndogo na gari la mizigo
“Basi lilikuwa likiipita gari ndogo iliyokuwa mbele yake, ghafla mbele kukawa na gari nyingine inayokuja, wakati huo huo kuna gari ya mizigo inafuata nyuma ya basi, hivyo ikaigonga kwa nyuma” amesema afisa huyo.

RAS Tabora awashukia wakurugenzi watendaji
Kaseja autaka utangazaji wa Radio/Tv