Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imethibitisha kupokea miili 20 ya watu waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ikihusisha gari ndogo aina ya IST, basi dogo Hiace na Lori.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Japhet Shani amesema Agosti 9 kuwa hospitali hiyo pia imepokea majeruhi 15 na kwamba wanaendelea kupokea matibabu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyanduhu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema uchunguzi unaendelea.

Endelea kufuatilia Dar24 Media kwa taarifa zaidi…..

Wakenya waishio Ughaibuni kupiga kura
Ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta kwa Wakenya