Takribani watu 20 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi kutikisa sehemu za kusini magharibi mwa mkoa wa Balochistan nchini Pakistan.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 katika kipimo cha Richter, limetokea eneo la karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iran kabla ya Alfajiri ya leo, wakati watu wakiwa bado wamelala.

Mamlaka ya taifa ya kukabiliana na maafa (NDMA) imesema watu kadhaa huenda bado wamenasa chini ya nyumba ambazo zimeanguka kwa sababu ya tetemeko la ardhi.

Waokoaji kutoka jeshini na mashirika ya kiraia wamesambazwa katika wilaya iliyoathirika zaidi ya Harnai na Umeme umekatwa katika maeneo mengi ya mkoa na hivyo kuvuruga shughuli za uokoaji na matatibu ya wale waliojeruhiwa.

Waratibu wa TASAF wapewa mwezi mmoja
Kocha Nabi aahidi furaha 2021/22