Watu 150 hawajulikani walipo baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Taarifa za tukio hilo kutoka Kivu Kusini zilizotolewa katika shirika la habari la Reuters, zimeeleza kuwa boti hilo ambalo lilikuwa limetoka katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini lilizama katika ziwa hilo karibu na eneo la Kalehe.

Miili mitatu iliopolewa, watu 33 wakaokolewa huku abiria wengine 150 wakiwa hawajulikani waliko kufuatia ajali hiyo.

Mara baada ya taarifa hizo, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Felix Tshisekedi ameeleza kusikitishwa na ajali hiyo, ambapo amesema atawachukulia hatua kali waliohisika na ajali hiyo.

”Nimehuzunishwa na kuzama kwa boti hiyo tarehe 15 mwezi Aprili katika ziwa Kivu. Hadi kufikia sasa idadi ya watu ambao hawajulikani waliko ni 150”. Amesema Rais Felix Tshisekedi kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Tshisekedi amesema kuwa anaifuatilia kwa karibu hali hiyo ili kuwatambua na kuwachukulia hatua wale waliohusika.

Video: Makonda kuwatimua wakuu wa idara wote wa Mkoa wa Dar es salaam
Video: Waziri Mpina azindua mafunzo kwa wavuvi, awatangazia neema wanaokula samaki
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 17, 2019

Comments

comments