Ajali mbaya imetokea katika eneo la Boko Magengeni jijini Dar es salaam, baada ya gari la mchanga kufeli breki na kugonga magari mengine ambapo watu watatu wamefariki na wengine kujeruhiwa.

Aidha, katika ajali hiyo bodaboda 20 zimeharibiwa huku magari 10 yakiharibiwa vibaya na Lori hilo la kubeba mchanga.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema jumla ya watu 3 wamefariki dunia huku watu 11 wakijeruhiwa.

Aidha, amesema kuwa jeshi la polisi pamoja na vyombo vyake linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo mbaya.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 8, 2018
Fahamu vigezo vilivyotolewa na HESLB kwa waombaji wa mkopo elimu ya juu

Comments

comments