Watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa vibaya , baada ya mlipuko wa bomu kutokea katika sherehe ya harusi katika mji wa Gaziantep, kusini mashariki mwa Uturuki
Gavana wa jimbo hilo, Ali Yer-likaya, ametaja shambulio hilo kama tukio la kigaidi mbalo haliwezi kuvumiliwa na mtu yeyote.
kwa upande wake waziri mkuu Mehmet Simsek, amesema kuwa mlipuko huo ni tukio la kinyama, huku akiongeza kuwa huenda lilitekelezwa na wapiganaji wa kujitoa muhanga
Aidha Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa kundi la Islamic State, ndilo lililotekeleza shambulio hilo la kinyama na lisilovumilika.
Ameongeza kuwa hakuna tofauti kati ya IS, Vuguvugu lililopigwa marufuku la PKK na wafuasi wa kiongozi wa kidini aliyeko uhamishoni nchini Marekani Fetullah Gulen, ambaye alilaumiwa kwa kupanga jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi uliopita