Watu 40 wamefariki dunia kufuatia mauaji yaliyafinyika baina ya wafugaji wa Hema na wakulima wa Lendu na kupelekea nyumba 1,000 kuchomwa moto kijiji cha Ituri Djugu, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Afisa wa Serikali amesema kuwa tayari wameitambua miili ya watu 30 waliofariki dunia kwa tukio hilo, huku zoezi la kutambua na kutafuta miili ya watu wengine likiwa bado linaendelea kufanyika maporini huko walikouawa.

Mwenyekiti msadizi wa kijiji cha Ituri Djugu, Willy Maese amesema nyumba 1,000 zimechomwa moto pindi kijiji hiko kilipovamiwa siku ya jumapili.

Mpaka sasa watu 130 wameuawa kufuatia matukio hayo ya mauaji yaliyoanzia kijiji cha Ituri mapema mwezi Disemba.

Mamia ya watu wametoroka kufuatia matukio hayo ya kikatili wakiwemo watu 27,000 ambao wamevuka mto Albert na kukimbilia Uganda.

Hata hivyo wiki ya pili ya mwezi Februari maelfu ya watu walikimbilia Uganda kwa  boti za kuvulia samaki na mashua huku wakiripoti kuwa majeshi ya wanaume wamevamia kijiji chao na kuua raia huku nyumba zao 1000 zikiwa zimechomwa moto kijiji cha Ituri’s Djugu.

Miaka mia iliyopita kumekuwa na ogomvi  kati ya wafugaji jamii ya Hema na wakulima wa Lendu na mauaji makubwa yalitokea kati ya  mwaka 1998-2003.

Miaka ya hivi karibuni makundi hayo mawili yamekuwa yakiendeleza mgogoro huo na kufanyiana matukio ya kikatili ya hapa na pale.

Mwaka jana ugomvi huo ulipelekea watu milioni 1.7 kutoroka Congo na kukimbia nyumba zao.

 

Shonza afunguka, amtaja Alikiba kuwa mfano wa kuigwa
Rais wa Mauritius Gurib-Fakim agoma kung'atuka