Watu 44 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa tuhuma za kutaka kuwauwa wanawake wanne kwa kuwachoma moto kutokana na imani za kishirikina.

Hayo yamesemwa hii leo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa ambapo amesema kuwa waliwakuta watuhumiwa hao wakiwasulubu wakina mama hao kwa bakora huku wakiwa wamewafunga kamba,

Amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kwenda kuwaokoa kina mama hao watuhumiwa walikimbia kwa kuhofia kukamatwa hivyo waliwachukua akina mama hao na kuwawahisha hospitali.

Aidha, Wanawake hao kwa sasa wapo katika hospitali ya rufaa ya Tabora walikokimbizwa na polisi ili kunusuru maisha yao kwa majeraha waliyoyapata, huku wakisema kama si jeshi hilo la polisi maisha yao yangekuwa yanaishia hapo.

Hata hivyo, Kamanda Willbrod amesema kuwa pamoja na watu hao 44 kukamatwa kuna wengine ambao walikimbia hivyo jeshi la polisi wanaendelea kuwasaka ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua.

Majaliwa atoa neno kuhusu watu wasiojulikana
Ligi daraja la pili kuanza Septemba 30, 2017