Watu watano wameatajwa kufariki katika shambulio lililotokea katika hoteli ya kifahari ya  Dusit iliyoko mtaa wa Riverside.

Shambulio hilo limetaja kundi la Al-shabab kuhusika na ufyatuaji wa risasi pamoja na utegaji wa mabomu yaliyolipuka katika eneo hilo na kudhuru watu kadhaa.

Shambulio hilo limefanywa na watu sita ambao walivamia majira ya leo saa 6 mchana.

Mbali na maiti hizo zilizobainika, shambulio hilo limesababisha idadi kadhaa ya majeruhi ambao tayari wapo katika mikono salama ya kuangaliwa afya zao.

Ambapo majeruhi watatu wamelazwa katika hospitali ya Agha khan na wengine watano wamelazwa katika hospitali ya MP Shah.

 

ICC yamuachia huru Rais wa zamani wa Ivory Coast
CCM Njombe wamng'ata sikio mwenyekiti wa chama hicho Iringa

Comments

comments