Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameripoti kuwa zaidi ya watu 60 wamezama baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama katika mto Congo.

Watu 300 wameokolewa lakini inakisiwa kuwa watu wengine 200 hawajulikani walipo baada ya ajali hiyo.

Wakazi wa eneo hilo wanasema boti hiyo iligonga mwamba mashariki mwa mji mkuu Kinshasa, wakati walipokuwa wakisafiri usiku.

Waziri wa Masuala ya Kibinadamu, Steve Mbikayi, ametaka wale wamiliki wa boti kushtakiwa na safari za majini nyakati za usiku zimepigwa marufuku nchini humo.

“Chombo kilichojaa kupita kiasi, kilichokuwa na abiria zaidi ya 700 kilipinduka Mai-Ndombe! miili 60 tayari imepatikana na watu 300 wamenusurika tunatoa pole kwa familia zilizofiwa na tunataka hatua zichukuliwa dhidi ya wale wote wanaohusika na sekta ya uchukuzi,” ameandika Waziri huyo kwenye mtandao wa Twitter.

Ibenge aomba kufutwa kazi AS Vita Club
Azam FC yamkataa Ndayiragije