Takribani watu 60 wameripotiwa kufariki dunia baada ya mabasi mawili kugongana usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kintampo kusini mwa Ghana.

Kamanda wa polisi, Antwi Gyawu ameliambia shirika la habari la AFP kwamba magari hayo yalikuwa yakitokea pande tofauti wakati ajali hiyo ilipotokea.

Aidha  Kamanda Gyawu amesema kuwa katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 60, basi moja lilishika moto huku jingine likiharibika vibaya, ambapo mabasi hayo yanakadiriwa kuwa yalikuwa yamebeba watu 50 kila moja.

Watoa huduma za dharura waliwasili katika eneo la tukio ikiwa ni pamoja na vikosi vya kuzima moto ili kuzima moto uliolipuka kutokana na ajali hiyo, huku miili 28 ikipelekwa kwenye hospitali ya serikali Kintampo kwaajili ya huduma ya kwanza kutokana na majeraha.

Dkt. Arhin ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 7 kati ya 28 waliofikishwa hospitalini hapo wako kwenye hali mbaya na wengine wamepata majeraha makubwa vichwani, na pia miili ya watu kadhaa waliofariki kwenye ajali hiyo imehifadhiwa Hospitalini hapo.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto wa eneo la Kitampo kulikotokea ajali hiyo Ankomah Twene, amesema abiria walionusurika wamesema kuwa dereva wao alikuwa akisinzia lakini abiria hao walipomsihi aweke gari kando kupumzika alikataa.

 

Video: UKAWA wamefanya kosa la KIHISTORIA | CCM wananufaika na migogoro ya Upinzani
Dkt. Bashiru awafunda CCM, 'Uhuni hautakiwi kwenye siasa'