Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta.
Watu hao wamekamatwa baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana.
Watu hao walikuwa wakiandamana kufuatia maandamano yaliyohamasishwa  kupitia mitandao ya kijamii yeye lengo la kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali.
Mbali na watu hao, baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam leo yamekuwa na watu wachache sana tofauti na siku nyingine za mapumziko, ambapo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutoka, kutokana na tetesi za kuwapo kwa maandamano.

Klabu ya Fulham kuumiliki uwanja wa Wembley
Wapigwa marufuku kutumia mtandao wa WhatsApp