Nusu ya watu Duniani, ambayo ni sawa ana asilimia 45 au watu bilioni 3.5 wanaugua magonjwa ya kinywa, huku watu watatu kati ya wanne walioathirika, wakiishi katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati huku Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, likibainisha kuwa, takriban visa vipya 380,000 vya saratani ya kinywa hugunduliwa kila mwaka.

Takwimu hizo, zinatokana na ripoti mpya ya hali ya afya ya kinywa duniani iliyochapishwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO ambayo inaeleza kuwa, visa vya kimataifa vya magonjwa ya kinywa vimefikia bilioni 1 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita ikiwa ni dalili ya wazi kwamba watu wengi hawana njia za kuzuia na matibabu ya magonjwa ya kinywa.

Kupiga mswaki husaidia afya ya kinywa. Picha ya Mtandao.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, “Afya ya kinywa kwa muda mrefu imekuwa ikipuuzwa katika afya ya kimataifa, lakini magonjwa mengi ya kinywa yanaweza kuzuiwa na kutibiwa kwa gharama nafuu ambapo WHO imetoa mwongozo na usaidizi ili watu wawe na maarifa na zana zinazohitajika kutunza meno na kinywa.

WHO inasema, athari zitokanazo na magonjwa ya kawaida ya kinywa ni kuoza kwa meno, ugonjwa ya fizi, kupoteza meno na saratani ya mdomo ambazo zimeathiri takriban watu bilioni 2.5 na wengi hawatibiwi ambapo ugonjwa wa fizi umetajwa kuwa ni sababu kuu ya kupoteza meno na unakadiriwa kuathiri watu bilioni 1 duniani kote.

Nitatumia bomu la Atomic: Kim Jong Un
Msimu wa Utamaduni SA na Tanzania umewadia