Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya Afya ya usikivu kwa wote hii leo, Shirika la Afya Duniani (WHO), limeonya kwamba robo ya watu Ulimwenguni kote (zaidi ya watu Bilioni 1) wanatabiriwa kuwa watapoteza kiwango fulani cha uwezo wa kusikia ifikapo mwaka 2050.

Kwenye ripoti yake ya kwanza ya Ulimwengu kuhusu hali ya kusikia iliyotolewa jana, WHO wanasema endapo hatua haitachukuliwa, basi watu wasiopungua Milioni 700 katika idadi hiyo, watahitaji huduma za kusikia au masikio kufanyiwa marekebisho.

Mkuu wa WHO, Dr. Tedros Adhanom amesema kutotibu tatizo la kupoteza uwezo wa kusikia, kunaweza kusababisha athari mbaya katika mawasiliano baina ya Watu.

WHO imekadiria kwamba watu Bilioni 1.1 walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 35 wako katika hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia kwa sababu ya kelele kuzidi sana katika mazingira.

Mazrui ateuliwa kuwa Waziri wa Afya Zanzibar
Tatizo la upumuaji lasababisha vifo vya Mapadri 25, Watawa 60