Watu 7 wamefariki dunia na watatu wamejeruhiwa, katika ajali iliyotokea eneo la Malendi Iramba mkoani Singida.

Taarifa zinaeleza kuwa watu hao ni pamoja na wafanyakazi wa Azam Tv waliokuwa katika safari ya kikazi, wakielekea wilayani Chato mkoani Geita kwaajili ya kuonyesha matangazo ya moja kwa moja kwenye shughuli ya TANAPA.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo gari dogo walilokuwa wamepanda wafanyakazi hao limegongana na lori lililokuwa likitoka Igunga kuelekea Dar es salaam.

Miongoni mwa vifo hivyo ni pamoja na wafanyakazi wa Azam Media, Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi, wengine ni dereva na utingo wake ambao majina yao hayajafahamika.

Majeruhi ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde ambao wapo ICU pamoja na Artus Masawe ambaye hali yake ni nzuri kiasi.

 

JPM atuma salamu za rambirambi Azam Media Limited
Timu ya taifa ya Marekani yatwaa ubingwa wa Wanawake