Taasisi ya Chakula na lishe imewataka watu waishio mijini waweze kuboresha lishe zao ili waweze kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Lishe, Sikitu Kihinga ambapo amesema kuwa ukiangalia data ambazo zipo kwasasa inaonyesha kwamba ishu ya uzito uliozidi iko kubwa katika mijini ukilinganisha na sehemu ya vijijini.

Amesema kuwa mtindo wa maisha uliopo kama vile kula vyakula vyenye mafuta yaliyozidi na kutokufanya mazoezi husababisha kuzidi kwa uzito na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.

“Tumekutana hapa ili tuweze kuangalia ni mikakati gani tunaweza kufanya kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba Lishe yetu inaimarika katika maeneo ya mijini, Watu wanaolisha watu mijini (Mama Lishe) kuna vitu mbalimbali ambavyo tunaweza kuwasaidia kwasababu tunaona watu wengi wanaoishi mijini huwa hawana muda wa kuandaa vyakula hivyo kuwalazimu kwenda kwa mamalishe,” Amesema Sikitu.

Aidha, ameongeza kuwa wameamua kukaa na Mama Lishe ili waweze kuona ni mikakati gani wanaweza kufanya na kuwasaidia ili kwamba wanahakikisha wanafanya Lishe kwa watu wanaoishi mijini kuwa vizuri.

Kwa upande wa Afisa mipango wa Shirika la Global aliance for improve Nutrition, Dkt. Winfrida Maila amesema  kuwa wanatakiwa kuweka mazingira mazuri kwa mama Lishe ili kuweza kuwashawishi watu wengi kupata chakula katika maeneo hayo.

Wajasiriamali waipigia goti serikali kuhusu vifungashio
LIVE MOSHI: Ibada maalum ya kuuombea mwili wa Dkt. Mengi

Comments

comments