Utafiti mpya wa kiafya umebaini kuwa watu warefu zaidi wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Saratani.

Kisayansi inadaiwa kwamba watu warefu wana seli nyingi mwilini hali ambayo inachangia kupata saratani .

Dr Leonard Nunney anasema watu walio katika mazingira ya kupata ugonjwa wa saratani iwapo tu atakuwa na ongezeko la urefu wa kawaida kwa kuanzia sentimita kumi.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa watu warefu kufikia kimo cha sentimita 178 ambao kwa mujibu wa utafiti huo wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kupata Saratani.

Ripoti ya utafiti huu mpya inakuja huku suala la uvutaji sigara likiendelea kutajwa kuwa chanzo kikubwa cha kupata ugonjwa wa Saratani kimo nacho ni sababu kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Takwimu za utafiti huu ziliwahusisha wanawake wapatao milioni moja kuangalia aina 23 za vimelea vya saratani katika nchi za Uingereza,Marekani, Korea Kusini, Australia, Norway na Sweden.

Kila kundi lililochaguliwa kufanyiwa utafiti lilipaswa kuwa na matukio 10,000 ya ugonjwa wa Saratani kwa kila jinsia.

Jumla ya aina 18 za Saratani zilifanyiwa uchunguzi kwa jinsia zote yaani wanaume kwa wanawake,ambapo ilibainika aina hizo za saratani hazina uhusiano na kimo kisicho cha kawaida cha kimo.

Wataalam wengine wanamashaka na matokeo ya utafiti huu na kudai kuwa kiwango cha sababu za urefu ni kidogo mno ikilinganishwa na sababu nyingine za ugonjwa huu kama vile uvutaji sigara.

 

Utafiti: Asilimia kubwa ya wanawake wenye vidole hivi huwa na mahusiano ya jinsia moja
Lukuvi apiga marufuku kudai kodi ya nyumba kwa miezi 6