Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya zoezi la kupima bure tezi dume (prostate) na mfumo wa njia ya mkojo kwa kutumia ultrasound.

Zoezi hilo limeandaliwa na Hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Matumizi ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wataalam wa mionzi tiba duniani.

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia, Dkt. Lulu Sakafu amesema kuwa umri unavyozidi kwenda juu, wanaume wanakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, hivyo wameshauriwa kujenga utamaduni kwa kupima afya zao mara kwa mara.

Aidha, amesema watu wasiofanya mazoezi wako katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, wanaume wanaopenda kula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta na wengine wanaweza pata ugonjwa huo kutokana na historia ya familia zao.

“Katika maadhimisho ya mwaka huu tumeamua kupima tezi dume kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 ili kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu kwa sababu kansa ya tezi dume duniani inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wanaume kutokana na saratani ya tezi dume,” amesema Dkt. Sakafu.

Hata hivyo, ameongea kuwa dalili za tezi dume, Dkt. Sakafu amesema kuwa kupata shida wakati wa haja ndogo, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza haja ndogo, kujisaidia mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku na kujikamua wakati wa kujisaidia na kushindwa kumali mkojo wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo amesema wanaume wasiogope kujitokeza kupima tezi dume kwa kuwa hivi sasa inatumika njia nyingine ya ultrasound badala ya ile ya zamani ya vidole.

Naye Rais wa TARA, Stephen Mkoloma ambaye ni mtaalam wa radiolojia amesema wamechangua kupima tezi dume kwa kuwa takwimu za wagonjwa wanaoripotiwa hospitali kutokana na matatizo ya tezi dume imeongezeka.

Video: Z Anto afunguka alivyojiweka rehani kuitetea nyota ya Diamond
Magari mawili ya serikali yagongana, saba wafariki