Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali ambayo imetokea eneo la Imezu wilayani Mbeya baada ya lori lenye namba za usajili T 616 DEX kuyagonga magari mengine mawili na kisha kupinduka.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya SACP Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano wa familia moja waliokuwa wakitokea msibani wilayani Mbozi mkoani Songwe kuelekea Morogoro.

Aidha kamanda Matei pia amewataja watu waliopoteza maisha pamoja na chanzo cha ajali hiyo huku akitoa wito kwa madereva kuwa makini kufatia ajari hizo kujirudia.

waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Tomas Mboya Sergent wa Jeshi la wananchi la Tanzania, Issabela Mbioya (53) mkazi wa Dar es Salaam, Magreti Masaki(22) mkazi wa Mbozi, Severina Mgaya na Joyce Mboya majeruhi katika ajali hiyo ni Eric Mboya ambaye yupo hospitali anaendelea kupatiwa matibabu chanjo cha ajali ni uzembe wa dereva mwenye gari namba T 616 DEX” amesema Kamanda Mtei

Young Africans yaweka rekodi 2020/21
Hatma ya Kombe la Dunia miaka miwili kujulikana