Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Afisa mtendaji wa Serikali ya mtaa wa Mbezi Msumi, Kelvin Mowo (38).

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema marehemu akiwa ofisini kwake anasikiliza mgogoro wa ardhi ghafla watu  wanne waliingia ofisini na mmoja  akatoa panga na kumshambulia mtendaji huyo kitendo kilichopelekea kupata majeraha makubwa na baadaye akapoteza maisha wakati akikimbizwa hospitali.

“Marehemu ni mkazi wa Bunju. Hivyo watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo wanahojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.Majina ya watuhumiwa hao kwa sasa yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi,” amesema Muliro.

Tukio hilo limetokea Oktoba 11, 2021 majira ya mchana eneo la Msumi Mbezi Wilaya ya Ubungo katika ofisi za Serikali ya mtaa.

Sadio Kanoute arudi kwa kishindo Simba SC
Tuchel arudisha jibu kwa Antonio Conte