Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa Diwani wa Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, amesema, watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

Lwena aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake Februari 22,.

Kamanda Matei amesema, kwa sasa majina ya watuhumiwa hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya upepelezi kukamilika.

Awali, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kamanda Matei, amesema, mauaji hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa Kata hiyo, Kennan Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016.

Amesema mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku kadhaa aliuawa.

Watalii wakatazwa kutoka kimahusiano na wazawa
Majaliwa: Ukikutwa na mwanafunzi wa kike nyumbani kwako jela miaka 30

Comments

comments