Watu 6 akiwemo raia mmoja wa Canada na mwanamke mmoja nchini Kenya wamefikishwa mahakamani kuhusiana na shambulio la kigaidi lililotokea jijini Nairobi katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 na kusababisha vifo vya watu 21.

Watuhumiwa hao wametambulika kwa majina kuwa ni Joel Ng’ang’a Wainaina, Oliver Kanyango Muthee, Gladys Kaari Justus, Osman Ibrahim, Hussein Muhamed na Guleid Abdihakim ambaye ni raia wa Canada.

Watuhumiwa hao mara baada ya kesi kusikilizwa watabaki chini ya ulinzi kwa muda wa siku 30 kupisha uchunguzi kuendelea.

Watuhumiwa hao wanashutumiwa kuhusu ‘uwezekano wa kuhusika’ katika shambulizi la takriban saa 20 kwenye hoteli ya Dusit D2 na jengo la ofisi ambalo mshambuliaji bomu wa kujitoa mhanga na watu wanne walio kuwa na silaha waliuawa na majeshi ya usalama, nyaraka iliyotolewa mahakamani imesema.

“Uchunguzi kuhusiana na suala hili una mambo mengi na ni wa kimataifa na huenda ukahitaji muda zaidi na rasilimali ili kubaini mtandao mzima wa kihalifu,” taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka, Noordin Haji imesema.

Washukiwa 11 walikamatwa Jumanne baada ya shambulizi, hata hivyo uchunguzi kuhusiana na washukiwa wengine bado unaendelea.

Mtuhumiwa Joel Ng’ang’a Wainaina ambaye ni dereva wa taxi anashutumiwa kwa kuwapatia usafiri washambuliaji mara kadhaa sehemu mbali mbali wakiwa mjini hapo mjini, na Muthee ni dereva mwingine ambaye aliwapeleka baadhi ya washambuliaji kwenye eneo la tukio.

Mwanamke pekee katika kundi hili la watuhumiwa Gladys Justus anachunguzwa kwa kuhusika katika kutuma fedha, wakati raia wa Canada, Guleid Abdihakim anachunguzwa kwasababu ya mawasiliano yake na baadhi ya watuhumiwa.

Ibrahim anadaiwa kuwa alikutana na mmoja ya washambuliaji Januari 8 huku Muhamed simu yake ilionyesha mawasiliano na baadhi ya wanamgambo wa kiislamu na atafikishwa mahakamani wiki ijayo siku ya Jumatano.

Washukiwa wawili bado hawajafikishwa mahakamani, Ali Salim Gichunge na Violete Kemunto Omwoyo ambayo wana kadi za simu ambazo zinaonyesha walikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na baadhi ya namba nchini Somalia, nyaraka za mahakama zimeonyesha.

Shambulizi ambalo inadaiwa lilifanywa na kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabaab la Somalia, lenye uhusiano na al-Qaeda limehusika kuilenga Kenya mara kwa mara katika mashambulizi.
Mwaka 2013 kundi hilo lilifanya shambuliz kwenye eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi na kusababisha watu 67 kupoteza maisha, wakati mwaka 2015 kundi hilo liliua watu 18 katika chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya.

Wabunge wa CCM wampongeza CAG
Mfahamu nyoka ‘Koboko’ hatari zaidi anaeuwa kwa dakika 3