Jeshi polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya dereva taks(uber) aliyefahamika kwa jina la Joseph Mpokala (51) ambaye ni mkazi wa Mbezi kwa Msuguri.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo ,watuhumiwa hao ni Godson Laurent, Sid Mohamed pamoja na Dennis Urassa, ambao wote wamekiri kufanya mauaji hayo.

Mnamo Mei 27, 2020 Godson alihojiwa na kukiri kufanya mawasiliano na marehemu ambapo alieleza kuwa mnamo Mei 21 2020 majira ya saa saba mchana walimkodi marehemu ili awapeleke maeneo ya Mbezi na walipofika Mbezi juu watuhumiwa hao walimuua Joseph Tilya na kumfukia kwenye shimo katika eneo la wazi lenye uzio wa ukuta ambao haujamalizika kujengwa.

Aidha baada ya kuhojiwa Juni 1 2020 watuhumiwa wote watatu walihijiwa kwa kina na kukiri kuwa walifanya mauaji hayo na kuchukua gari alilokuwa akiendesha marehemu aina ya IST yenye namba za gari T139 DST na kulificha huko kimara barutri katika numba ya wageni ya Api Forest Lodge.

Hata bhivyo ,jeshi hilo lomesema kuwa linakamilisha taratibu za jalada kwa mwanasheria wa serikali na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Inaelezwa kuwa mnamo Mei 26, 2020 ” jeshi la polisi kanda maalumu ilipata taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa mume wake ametoweka tangu Mei 21,2020 na simu zake zote hazipatikani.” ndipo wakaanza uchunguzi.

Gadiel Michael: Sijapotea njia, ninapenda ushindani
UCHUNGUZI WA AWALI: Takukuru wabaini matumizi mabaya fedha za AFCON