Mtandao wa Instagram upo mbioni kuanza kuweka matangazo kwenye video za IGTV na kuwapa fursa watumiaji wake kuanza kutengeneza pesa.

Kwa mujibu wa Hollywood Report, kampuni hiyo inataka kutambulisha Updates na Features mpya ambazo zitawanufaisha na kuwafanya watumiaji wake wajitengenezee pesa Kama ilivyo kwa YouTube .

Justin Osofsky, CEO wa Instagram, amesema kuwa Lengo la kufanya hivyo ni kujaribu kupanua kampuni na kuifanya kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani.

Imeelezwa kuwa Instagram itashiriki kwa kukata asilimia 55 kutoka kwa muhusika wa maudhui.

Aidha moja Kati ya mabadiliko hayo makubwa , ni pamoja na kuweka matangazo kwenye video ndefu zinazozidi sekunde 60 (InstagramTv) . Pamoja na Beji za makampuni kwenye Insta Live , ambazo zitamfanya aliyeweka video hizo kulipwa.

Osofsky ametoa ufafanuzi juu ya maudhui ambayo yatakuwa yanawekewa matangazo kwa ajili ya malipo niyale ya muhusika na kutolea mfano maudhui ambayo mtandao wa Yotube haulipii ingawa amesema kuwa Instagram itajitahidi kuwa na malipo makubwa kuliko Youtube,

Mbaraka Yusuph aahidi kupambana Azam FC
Kikwete athibitisha usalama Hosteli zilizotumika karantini UDSM