Vyombo vya habari vinavyorusha maudhui yake kwa njia ya mitandao ya kijamii vimetakiwa kuzingatia weledi na ubunifu ili kulifikia soko kubwa la watumiaji wa mitandao hiyo.

Mkufunzi Mwandamizi wa masoko na biashara kwa njia ya mitandao ya kijamii, Dotto Mnyadi amesema ongezeko la watumiaji wa mitandao ya kijamii na intaneti nchini ni fursa kwa vyombo vya habari kuuza maudhui yao kwenye mitandao hiyo na kujinufaisha kiuchumi.

Ameyasema hayo wakati wa mafunzo maalumu kwa wanahahabari yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya ambayo yanafanyika Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni kuwa robo ya watanzania wanatumia mitandao ya kijamii na asilimia 90 kati yao wakitumia simu zao za mkononi kuingia katika mitandao hiyo huku idadi ya watumiaji wa mitandao hiyo ikipanda kutoka milioni 17 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 29 mwezi machi, mwaka 2021.

Wananchi wailalamikia serikali kuhusu waraibu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 12, 2021