Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI,  imefanikisha kufanya uthibiti wa uchepushaji wa madawa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2  uliofanywa na mafamasia wa kitengo hicho kwa matumizi yao binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, amesema kuwa madawa hayo waliyachepusha kupitia mfumo wa kutunza taarifa za kumbukumbu za madawa MEDPRO4.

Akieleza namna ubadhirifu huo ulivyofanyika Mbungo amesema kuwa, mafamasia hao walikuwa wanaongeza idadi ya dawa kwenye cheti cha mgonjwa tofauti na idadi alizoandikiwa na daktari na pia kuongeza dawa zenye fedha kubwa kwenye fomu za madaktari.

Mbungo amesema mpaka sasa watumishi 23 wa MOI kitengo cha Famasi wanaendelea na mahojiano TAKUKURU.

Sambamba na hilo TAKUKURU imezindua TAKUKURU mobile  (Mtandao unaotembea) mikoa yote nchini kwa lengo la kutatua changamoto za wanachi zinazowakabili ambapo kila mkoa inaratiba yake.

TAKUKURU inaendelea na kampeni za uokoaji mali zikiwemo za serikali na taasisi binafsi.

Bofya hapa.

Uganda kufanya maamuzi
Onyango aipongeza Young Africans