Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, Dodoma imesema watumishi wote waliondolewa katika utumishi wa umma kwa sababu ya kukosa vyeti vya kidato cha nne hawana madai yoyote serikalini.

Kauli hiyo imetolewa leo na kaimu Katibu Mkuu Katika Ofisi hiyo, Mathias Kabunduru katika kikao cha wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa wizara zote, makatibu tawala, wasaidizi mkoa na mkuu wa idara za utumishi na utawala.

Amesema zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma lilihitimishwa Oktoba, 2017 na wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne waliambiwa waondoke kwa hiari yao.

Hata hivyo amesema bado watumishi wasio na vyeti hivyo wako kazini kama ilivyobainika katika Wilaya ya kwimba.

Amewataka maofisa utumishi kuwaondoa wale waliobaki kwa sababu watakapowagundua wataadhibiwa wao na wakurugenzi wao.

”Muwaondoe wote katika orodha ya mishahara na watakaondolewa wote hawana madai yoyote serikalini,” amesema Kabunduru.

Watumsihi hao waliokosa sifa pamoja na wale waliobainika kuwa na vyeti bandia waliagizwa kujiondoa wenyewe kwenye utumishi wa umma mwaka 2016, ambapo Rais John Magufuli aliazisha vita dhidi ya wafanyakazi waliokosa sifa ambao walikuwa serikalini.

Edo Kumwembe ampa ufalme John Bocco
Subalkheri kuwatia mahakamani Aslay na Nandy