Aliyekuwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Tabora Mohamed Abdallah na Muhandisi Mwandamizi, Melkiad Msigwa wamefikishwa mahakamani kwa makosa saba ikiwemo la uhujumu uchumi na kuisabishia serikali hasara ya shilingi milioni 60.

Makosa hayo yalifanyika kati mwaka 2015 na Novemba 2018, ambapo Mohamed na Msigwa walitenda makosa kwa kuendesha genge la uhalifu.

Aidha Muhandisi Msigwa alighushi risiti kuonyesha amenunua vifaa vilivyoorodheshwa kwenye risiti wakati wa ujenzi wa mradi wa kituo cha kupozea umeme kwenye mizani ya Puge Wilaya ya Nzega.

Kati ya Machi mwaka 2016 na Mei 2018 akiwa Meneja Mohamed alitumia madaraka yake kufanya maamuzi ya kujenga mradi wa kusambaza umeme kwenye mizani ya Puge, kazi ambayo tayari iliidhinishwa na Wakala wa Barabara TANROADS ifanywe na M/S Mawenji Electrical Contarctor na kujipatia kiasi cha milioni 20.

Biden ashiriki mkutano wa Munich
Ndugulile atangaza 'kiama'