Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbung’o, amewasimamisha kazi watumishi Tisa ambao walihusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo Saba ya Taasisi hiyo yaliyojengwa Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

Hayo yamejiri zikiwa zimepita takribani saa kadhaa baada ya Rais Dkt. John Magufuli kueleza kutoridhishwa na gharama ya ujenzi wa ofisi hizo zikilinganishwa na ubora na muonekano wake.

Jana wakiti akizindua mradi wa ofisi za TAKUKURU Chamwino jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema mradi huo haukuwa wa yeye kwenda kuufungua lakini akiangalia vizuri thamani hiyo ni ya juu sana na kuongeza amejenga nyumba yenye ukubwa kama huo huko kwao kwa Milioni 40.

“Nahili siwezi nikalificha, ndiyomaana nimezunguka hivi nikaangalia nikasema hamna hapa tumeliwa, nikazungumzie wapi? ofisini, hapahapa ili brig. jenerali ujue” alisisitiza Magufuli

Azam FC waanika sababu ya kuitaka nafasi ya pili VPL
Dodoma: Kiongozi wa CHADEMA auawa kwa mshale