Watumishi wa umma nchini wametakiwa kuwa tayari kwenda kufanya kazi kokote watakapopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika, kwani moja ya wajibu wa watumishi wa umma ni kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania sehemu yoyote walipo ili kuwaletea maendeleo na atakayeshindwa ni vema akatafuta shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

Hayo yamesemwa na waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa  Septemba 23, 2016 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mkunguni wilayani Mafia.

Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

Amesema hii ni awamu ya kazi zaidi ambapo hata kauli mbiu ya Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu! si neno la kufurahisha bali lina malengo yanayowataka Watanzania wote wafanye kazi, kwani kila awamu inakuwa na mkakati wake, watumishi wa umma wanatakiwa kubadilika na kufanya kazi kutokana na awamu iliyoko madarakani inavyotaka.

Majaliwa atembelea kiwanda cha samaki TANIPESCA
Ziara ya Lowassa Kagera yazua gumzo, afikisha kilio chake kwa Mkuu wa Mkoa