Serikali imewawezesha watumishi zaidi ya 2000 kumiliki nyumba bora kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu na kuchangia kuongeza tija katika utumishi wa umma.
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Nyumba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Michael Mwalukasa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
 Mwalukasa amesema kuwa kupitia Mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali watumishi wengi walioomba mikopo hiyo wameweza kupewa kwa lengo la kuwawezesha watumishi wa Serikali wa ngazi zote mijini na vijijini kujenga, kukarabati au kununua nyumba.
 “Mfuko huu umewawezesha watumishi wa Serikali kujenga nyumba kwenye maeneo yenye hadhi na yanayokubalika kisheria hivyo kuchochea kasi ya maendelezo ya nyumba kwenye Miji na Wilaya zote hapa nchini” amesema Mwalukasa.
 Hata hivyo, Mwalukasa amesema kuwa watumishi wanaokopa kwenye mfuko huo hurejesha mikopo hiyo kwa riba nafuu ya asilimia tatu tofauti na taasisi nyingine ambazo hutoza riba kubwa.
 
Bocco: Young Africans Ina Kikosi Bora
Maelfu yamiminika kulipa deni Bodi ya Mikopo, picha za wadaiwa kuanikwa