Watumishi wa umma tisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma wamekumbwa na nyundo ya mtumbua majipu na kusimamishwa kazi kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma (RAS – Kigoma), John Ndunguru aliwaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi huo umechukuliwa kufuatia maagizo ya waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa baada ya kubaini ubadhirifu huo alipofanya ziara mkoani humo.

Ndunguru alieleza kuwa uongozi uliunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi na kubaini kuwa watumishi hao walihusika moja kwa moja katika ubadhirifu wa fedha za umma kwa kufanya manunuzi hewa ya shajala yenye thamani ya shilingi milioni 4, vipuri vya shilingi milioni 8 pamoja na ubadhirifu wa fedha za umma.

Aliongeza kuwa, watumishi hao pia walihusika kuinyima serikali mapato kwa kuuza majengo ya Kigodeco na Mibox kwa bei ya chini isiyo halali ya shilingi milioni 370 badala ya shilingi milioni 470.

Aliwataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Willyfred Mwita (Afisa Mipango), Emmanuel Mkwe (Mwanasheri), Boniface William (Mhandisi wa Manispaa), Musa Igugu (Afisa Biashara), Elimboto Zakaria (Mkaguzi wa ndani), Leonard Nzilailunde (Afisa Ugavi) Shida Tadei (Mhasibu), Omary Lubibi (Fundi Mkuu wa Magari) na Mawili Mkoko.

Mashabiki wa Ali Kiba waivimbia MTV Base
Benitez Ajipaka Mafuta Kwa Mgongo Wa Chupa