Watumishi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia mbinu mbalimbali za kiutendaji kazi ili kuweza kuifanya Wizara kujulikana na kuleta maendeleo katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana na wafanyakazi wa Wizara hiyo jana Jijini Dar es Salaam.

Prof. Gabriel amesema kuwa jamii itathamini kazi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama Watumishi wa Wizara watafanya jitihada za makusudi kwa kuwa wabunifu katika utendaji kazi hivvo kuleta tija na heshima kwa Serikali.

“Ni vema kila Mtumishi akajituma katika kukamilisha majukumu ya Wizara yetu kwa kasi na kwa wakati huku tukithamini maslahi ya jamii tunayoitumikia” alisema Prof. Gabriel

Aidha Prof. Gabriel amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuheshimiana na kuishi kama ndugu kwani muda mwingi hutumia wakiwa ofisini na kuwahaidi kuwa kwa upande wake atahakikisha kuwa Watumishi wote wanaishi katika mazingira rafiki katika eneo la kazi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Magreti Mtaki amewataka watumishi wa wizara kuacha kungojea fursa zinazopatikana nje ya Wizara bali kutumia fursa zinazopatikana ndani ya Wizara kwani ni rahisi kuzisimamia na kuziendeleza kwa maendeleo ya Taifa letu.

mwisho

Hospitali Ya Siha Mkoa Wa Kilimanjaro Watatua Tatizo La Dawa
Kesi Ya Tundu Lisu Yapigwa Kalenda