Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewataka Watunza Kumbukumbu na Nyaraka katika taasisi za umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujiepusha na uvujis wa siri za serikali.

Mchengerwa ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 9 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania katika ukumbi wa ACC jijini Arusha.

Mchengerwa amesema, dhamana waliyonayo Watunza Kumbukumbu ni kubwa, hivyo ni vema wakazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za utunzaji wa kumbukumbu pamoja na viapo vyao kwasababu utoaji wa siri za Serikali ni kosa kubwa kisheria na kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma.

Mchengerwa amesisitiza kuwa, Serikali ya Awamu Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inathamini mchango wa Watumishi wa Umma na itaendelea kulinda maslahi yao ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili Watunza Kumbukumbu, hivyo hakuna sababu ya watumishi kutoa siri za Serikali na badala yake wanapaswa kuwa waadilifu kiutendaji na kuwa watiifu kwa Serikali yao.

Amewaagiza waagiza waajiri wote kuhakikisha wanalipa stahili zote za watumishi ikiwepo madai ya malimbikizo ya mishahara na kuongeza kuwa wanapaswa kutenga muda wa kusikiliza kero za watumishi na kuzitafutia uvumbuzi.

Akizungumzia juu ya stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma, Mchengerwa amewaagiza waajiri wote kuhakikisha wanalipa stahili zote za watumishi ikiwepo madai ya malimbikizo ya mishahara na kuongeza kuwa wanapaswa kutenga muda wa kusikiliza kero za watumishi na kuzitafutia uvumbuzi, huku akisisitiza kuheshimu waajiri kuheshimu kada zote kwani kila kada ina umuhimu wake katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Rais Samia amtembelea Waziri mstaafu Lowassa
Biashara United yakana tuhuma za rushwa