Mtendaji mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke, amefungua milango kwa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, kwa ajili ya kulimaliza suala la usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Aubameyang amekua katika minong’ono ya kutaka kuihama klabu hiyo tangu mwishoni mwa msimu uliopita, lakini ukimya wa viongozi wa Borussia Dortmund ulizima mipango hiyo, kufuatia kutotaka kujihushwa moja kwa moja.

Klabu za Man City, Real Madrid, Chelsea na Juventus zilitajwa katika vyombo vya habari kuhusu uwezekano wa kumsajili Aubameyang lakini bado alibaki Signal Iduna Park.

Usiku wa kuamkia hii leo, Watzke alihojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Deutschland na alieleza dhamira waliyoiweka katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu kuhusu fununu za kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

“Endapo Real Madrid wataonyesha nia ya dhati ya kutaka kuzungumza nasi kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang, tutakua tayari kufanya hivyo.

“Najua yatakua mazungumzo ya awali na tutafanya hivyo kwa ajili ya kufanya biashara, Pierre-Emerick Aubameyang ana mkataba na Borussia Dortmund hadi mwaka 2020, hivyo hakuna haja ya kuliharakisha suala hili, zaidi ya kuacha mazungumzo yafanye maamuzi lakini endapo watakua tayari kuja kwetu na kutueleza dhamira yao.

“Hatuna haraka na jambo hilo kwa sababu tunafahamu soka ni biashara na inapojitokeza ni lazima ifanyike bila kuwekwa kizuizi.

“Kwa sasa tunamuachia rais wa Real Madrid Florentino Perez.” Alisema Watzke

Majaliwa atoa mwezi 1 kwa Mkurugenzi Nachingwea kutumia mfumo wa Kielektroniki
Arsene Wenger: Mesut Ozil Bado Ana Ndoto Za Kuitumikia Arsenal