Mtendaji mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amesema ilikua ni vigumu kwa klabu hiyo kugoma kumuuza kiungo mshambuliaji kutoka nchini Almeria, Henrikh Mkhitaryan aliyejiunga na klabu ya Man Utd mwishoni mwa juma lililopta.

Watzke, amesema Man Utd waliwasilisha ofa ya Euro milioni 42, ambayo iliwavutia na wakaona kuna umuhimu kwa kiungo huyo kuondoka na kwenda kuanza maisha mpaya ya soka lake nchini England.

Amesema Mkhitaryan alikuwa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na ofa hiyo ilikua kubwa tofauti na walivyofikiria, hivyo hawakufikiria mara mbili suala la kumruhusu kuondoka.

Henrikh Mkhitaryan

“Uhamisho wa Mkhitaryan umekua na faida kubwa sana kwetu, hatukutarajia kama tungeweza kumuuza kwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kiliwasilishwa kwetu na Man Utd” Alisema Watzke

Mkhitaryan anaingia katika mipango ya meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho, ambaye amedhamiria kukisuka upya kikosi mashetani wekundu ambacho kimekua hakifanyi vyema tangu alipoondoka Sir Alex Fugerson.

The Eagles Wajipanga Upya Kwa Christian Benteke Liolo
Pep Guardiola: Sina Mpango Wa Kumsajili Lionel Messi