Serikali imeombwa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waganga wa kienyeji ambao  watakutwa na makosa yanayohusiana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, katibu wa Baraza la waganga BAWATA Shariff Karama amesema wapo baadhi ya wahalifu wanaotumia mwamvuli wa waganga wa kienyeji na kufanikiwa kutekeleza unyama huo.

Aidha  BAWATA imeitaka serikali kutokuwa  na kigugumizi kuwaangalia waganga wasiosajiliwa kwani na hao wanatoa tiba hivyo wanatakiwa wawe na vyeti na wajulikane kihalali juu ya ufanyaji wa kazi zao.

DSC_0869

Pamoja na hayo wameitaka serikali kuwachukulia hatua stahiki waganga wanaojitangaza sehemu mbalimbali pasipo kufuata taratibu za kupimwa kwa madawa yao kama kweli zinasaidia watu.

Hata hivyo katibu Sharrif amesema kuwa bajeti  ya wizara ya afya haijagusa kusaidia waganga wa tiba asili hasa katika suala zima la kukuza taaluma ili iweze kuwaingizia serikali mapato.

Bawata imependekeza serikali kutengeneza viwanda vya usindikaji wa dawa za tiba asili kwani kwa wingi wao serikali ingeingiza mapato makubwa pia kupunguza suala la ukataji miti hovyo nchini.

Pamoja na hayo katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya tiba asili tanzania SHIVYATIATA, Othman Shemu amesema kwamba  BAWATA kushirikiana na shirikisho wamepiga marufuku upigwaji ramli mpaka hapo watakapotoa tamko kutokana kashfa dhidi ya watoaji wa huduma hiyo.

DSC_0868

Amesisistiza kuwa kwa sasa upigwaji wa ramli unahusishwa moja kwa moja na mauaji ya watu wenye ulemavu wa  ngozi hivyo wananchi waonapo hali hiyo watoe taarifa.

hata hivyo Bawata itafanya mkutano wa hadhara Songea kwa ajili ya kuipongeza serikali kwa jitihada za kazi lakini pia kwa ajili kuonya waganga matapeli, wabakaji na wale wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya Albino.

 

 

 

Unyama: Majambazi yawaua kinyama watu wanane na kuiba sukari, Biskuti
Wanafunzi wa UDSM wagoma, Bodi ya Mkopo yakwamisha ahadi ya Magufuli