Mtu mmoja aliyekuwa nusu uchi amewaua watu wanne katika mgahawa mmoja huko Nashville katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.

Mtu huyo alianza kuwamiminia risasi watu waliokuwa katika hoteli hiyo na bunduki yake ambapo pamoja na kuwaua watu hao lakini pia amewajeruhi wengine wawili.

Polisi wanaendelea kumsaka mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Travis Reinking mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Illinois.

Aidha, Don Aaron amesema kuwa Travis mwaka jana aliwahi kushikiliwa na Polisi pale alipojaribu kuingia katika eneo ambalo lipo karibu na Ikulu ya Marekani lenye kizuizi.

Hata hivyo, James Shaw mmoja wa wateja katika mgahawa huo amepongezwa kwa ujasiri wake,aliouonyesha baada ya kumnyang’anya bunduki mshambuliaji huyo ambaye huenda bila hatua hiyo angesababisha vifo vya watu wengi zaidi.

Sheria ya umiliki wa silaha nchini Marekani bado inatoa mwanya wa kuzagaa kwa silaha hali ambayo imekuwa ikisababisha mashambulizi ya mara kwa mara ya silaha zinazomilikiwa na watu kwa urahisi.

Baba Masogange ataja ahadi ya mwisho ya mwanaye
Video: ACT yamficha Zitto Kabwe, Utabili hali ya upinzani 2020

Comments

comments