Huduma za matibabu zimesimama katika kaunti 11 nchini Kenya, kufuatia mgomo wa kufanya kazi wa wauguzi ulioanza mapema leo.

Wauguzi hao wamegoma baada ya kukamilika kwa muda waliokuwa wameipa Serikali kufanyia kazi makubaliano kati yao ya Desemba mwaka jana, ambayo yalitoa nyongeza ya stahiki na kupandishwa madaraja.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi cha Kenya (KNUN), Seth Panyako ameiambia Citizen kwenye mahojiano maalum kuwa wauguzi kwenye kaunti 11 hawatafanya kazi.

“Mgomo unaendelea katika kaunti 11 na kama tulivyokuwa tumesema awali mgomo wetu unafanikiwa sana,” Panyako amesema.

“Notisi ya mgomo ilitolewa kwa kila Serikali ya Kaunti husika. Makubaliano ya kurejea makazini ya Desemba mwaka jana hawakuyafanyia kazi. Maombi ya wauguzi katika kila Kaunti ambayo mgomo unafanyika yanapaswa kujibiwa na kaunti husika,” aliongeza.

Alitoa mfano wa malalamiko ya wauguzi katika Kaunti ya Nairobi, alisema kuwa wauguzi hawajapandishwa madaraja kwa takribani miaka sita.

Kaunti ambazo zimeathirika na mgomo huoni T Nairobi, Kisumu, Homa Bay, Muranga, Kisii, Embu, Kiambu, Garissa, Elgeyo Marakwet, Kirinyaga, Marsabit, Nyandarua na Nyer.

Nyingine ni mburu, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia, Tharaka Nithi, West Pokot, Kitui, Wajir, Kwale, Mandera pamoja na Taita Taveta.

Waganga wa Jadi wawekwa kitimoto mkoani Njombe
Makamu wa Rais atoa neno baada ya kupata ajali ya ndege