Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Bi. Ziada Sellah amewataka Wauguzi na wakunga kuwa na lugha nzuri na ubunifu wakati wa kuwahudumia wagonjwa Hospitalini, kwani vitendo hivyo haviendani na maadili ya taaluma yao.

Bi. Sellaa ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wakiwemo wauguzi wa afya na kuongeza kuwa, baadhi ya Wauguzi na Wakunga kujikuta wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa jambo linaloweza kuharibu taswira ya taaluma hiyo.

Mkurugenzi huduma za Uuguzi na Ukunga, Ziada Sellah. (Katikati)

Amesema, “Fanyeni kazi ya uuguzi na ukunga kwa moyo wote, kumekuwa hakuna kauli nzuri kwa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wetu wetu pindi wanapokuja katika Hospitali zetu, maana kumekuwa na tabia chafu ya baadhi ya Wauguzi na Wakunga kujikuta wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa hii haifai.”

Aidha Bi. Ziada ametoa wito kwa Wauguzi kujiendeleza kielimu ili waweze kujiongezea maarifa na utaalamu wa kutoa huduma bora na zenye tija kwa wagonjwa na kuwaasa watumishi wa sekta ya Afya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano, huku wakizingatia suala la uwazi.

Papa Francis akutana na Sheikh Ahmed al-Tayeb
Maandalizi urejeshaji madhari ya Misitu yakamilika