Waumini 44 wa parokia moja ya Kanisa la St. Peter’s la Manhattan nchini Marekani, wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kupata maambukizi ya virusi vipya vya corona (covid-19).

Kwa mujibu wa CNN, Mchungaji wa parokia hiyo, Fabian Arias na viongozi wengine wa kanisa hilo wamesema kuwa waumini hao ni pamoja na waliokuwa wahudhuriaji wa siku zote na wale waliokuwa wanafika kanisani hapo kwa matukio maalum kama ubatizo na sikukuu.

Viongozi hao wa kanisa waliipa timu ya CNN nakala ya majina ya waumini hao ili iweze kufuatilia na kuthibitisha, ingawa walitoa masharti ya kutoweka hadharani majina hayo.

Chombo hicho cha habari kimeeleza kuwa kimefanya ufuatiliaji wa kina kwa kutumia majina yaliyopewa; na kwa awali tu walibaini theluthi ya majina hayo yalikuwa pia kwenye orodha ya majina yaliyowekwa kwenye kumbukumbu za serikali za waliopoteza maisha kwa covid-19.  

Kanisa la St. Peter’s hupokea waumini kutoka katika maeneo mengi ya New York, na wengi huingia kanisani wanapotoka kazini.

Waumini wengi wa kanisa hilo ni wenye asili ya Latino (Latin America). Viongozi hao wameeleza kuwa kanisa hilo liliwavutia wahamiaji wengi kwakuwa hutoa pia huduma kwa lugha ya Kihispania.

Askofu Paul Egensteiner ambaye alichaguliwa mwaka jana kuliongoza Kanisa la Evangelical Lutheran’ Metropolitan la New York, amesema kuwa waumini wengi wenye asili ya Latino katika jiji hilo wameshambuliwa zaidi na covid-19. Baadhi ya Wachungaji wameripotiwa wakieleza kuwa kati ya 25% na 30% ya waumini wao wamepata maambukizi ya virusi vya corona.

Watu wenye asili hiyo wanaoishi jijini New York wameripotiwa kuwa wameathirika zaidi na virusi vya corona. Hadi kufikia Mei 6, 2020 zaidi ya watu 5,200 wenye asili ya Latino walifariki kwa virusi hivyo.

Kanisa hilo lilifungwa kwa muda tangu Machi, 2020 kutokanana na tishio la virusi vya corona. Mchungaji Arias anaendesha ibada kwa njia ya mtandao akiwa sebuleni kwake, Bronx nchini Marekani.

Visa vya corona vyafika 737, visa vipya 22 vyabainika – Kenya

Ibada ya mazishi yashambuliwa kwa mabomu, 24 wafariki

Madereva 23 wa Tanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na virusi vya corona
Waombolezaji washambuliwa kwa mabomu, 24 wafariki