Wafanyakazi wa migodi wamevamia shamba la mke wa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Grace Mugabe na kuanza kuchimba dhahabu.

Kwa mujibu wa gazeti la Newsday la Zimbabwe, watu hao walikutwa waking’oa mazao kisha kuanza kuchimba mchanga na mashimo wakipakia kwenye lori kwa ajili ya kuchekecha wapate madini.

Imeripotiwa kuwa Mama Grace aliyefika hapo na kushindwa kuelewana na watu hao aliamua kuripoti katika kituo cha polisi.

Shamba hilo liko Mazowe, eneo ambalo awali lilikuwa linakaliwa na wanakijiji kabla ya kuondolewa mwaka 2015 enzi za utawala wa Mugabe.

Kupitia taarifa aliyoitoa polisi, Mama Grace alisema kuwa alikuwa anatembelea shamba lake lakini alishtuka kuona watu zaidi ya 400 wakiwa wanaharibu mazao na kuchimba mashiko kutafuta dhahabu.

Alisema alipojaribu kuwakataza walimzomea na kumueleza kuwa hana mamlaka tena ya kuwaondoa.

Meya wa jiji atekwa nyumbani kwake
Katibu wa Chadema aachia ngazi, ajiunga na CCM

Comments

comments