Wavuta sigara wa jijini London nchini England wamepewa nafasi ya kuchagua mchezaji bora wa dunia kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Jijini humo pamefanyika ubinifu kwa kushirikiana na wanamazingira kwa kuwashurutisha wanaotumia sigara kutupa vichungi vyao kwenye ubao maalum uliobeba maboksi.

Mbao hizo zimewekwa sehemu mbalimbali jirani na barabara na hali hiyo imeandaliwa ili kupunguza wingi wa vichungi vya sigara vilivyokuwa vinatupwa barabarani hovyo.

Lakini inaaminika itawasaidia wavuta sigara wakati mwingine kutomaliza sigara yote kama wataviona viboksi hivyo kwa kuvitupia ili kupiga kura ingawa haitahusisha Fifa au kuwasaidia Ronaldo au Messi kushinda kweli.

Utaratibu huo wa utunzaji wa mazingira umekua ukichukua nafasi kubwa kupitia michezo ya soka ama ushindani wa kisiasa ambapo majina ya wachezaji, timu ama vyama vya siasa huwekwa sehemu mbili tofauti na kushindanishwa na vichungi vya sigara.

Angalia mbao hizo siku za nyuma ziliwahi kuwa na majina haya.

 

Berbatov Akabidhiwa Jezi Namba 10 PAOK Salonika
Misri Yaanza Kurejea Kwenye Ubora Wake